24 Juni 2026 - 16:01
Sheikh Naim Qassem: Mpango wa Kuangamiza Iran na Muqawama Umeshindwa / Amani Itategemea Kusitishwa kwa Uvamizi na Kujiondoa kwa Adui

Katibu Mkuu wa Hezbollah amesema kuwa mpango wa kuangamiza Iran na muqawama umefeli, akisisitiza kuwa kusitishwa kwa mapigano lazima kuwe kwa masharti ya kusitishwa kabisa kwa uvamizi na kujiondoa kwa adui katika maeneo wanayoyakalia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Katibu Mkuu wa Hezbollah, Sheikh Naim Qassem, amesema kuwa mabadiliko ya sasa yanaonyesha kushindwa kwa kile alichokiita “mpango wa kuangamiza Iran na muqawama.”

Amesisitiza kuwa kubaki kwa Israel katika ardhi ya Lebanon ni jambo lisilowezekana, akisema hakuna eneo lolote la “usalama” linaloweza kudumu kwa upande wa Israel ndani ya Lebanon.

Sheikh Qassem pia ameitaka Marekani kukomesha mradi wa Israel katika eneo hilo, akisisitiza kuwa Israel ni mvamizi na inapaswa kuondoka kikamilifu katika maeneo yote inayoyakalia.

Aidha, amesema anaamini kuwa Israel itakabiliwa na kuporomoka kutoka ndani, akieleza kuwa vitendo vyake vya sasa ni uonevu unaovuka mipaka ya uvumilivu wa binadamu na unaendelea kuzidisha mivutano katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha